Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uturuki

Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uturuki litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu (BOT) kuanzia saa nane mchana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, pamoja na Rais wa uturuki Mhe. Recep Tayyip ERDOGAN, Kongamano hilo litawakutanisha wafanyabiashara kutoka Uturuki pamoja na wafanyabiashara kutoka nchini Tanzania kwa lengo la kuweka ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili.