Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

African Organization for Standardization(ARSO) ‘MADE IN AFRICA’ EXPO 20th–24th JUNE,2016 IN ARUSHA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF), Wanawaalika wazalishaji wote kujiandikisha kushiriki katika mashindano ya bidhaa 50 bora zinazozalishwa Tanzania na katika Maonesho ya bidhaa za kiafrika "ARSO Made in Africa Expo" ambayo yatafanyika jijini Arusha kuanzia Juni 20 hadi 24, 2016. Mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi ya maonesho ya bidhaa bora za kiafrika yatakayofanyika katika ngazi ya bara nchini Misri mwaka 2017. Ushiriki katika maonesho hayo ni fursa na jukwaa la kujenga mtandao wa maingiliano baina ya jumuiya ya wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, kuvutia wawekezaji katika sekta ya Viwanda na kupata muda kuonesha bidhaa wakati wa mkutano na Baraza la Arso. Kwa Mawasiliano zaidi: Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Viwango Tanzania, S. L. P 9524, Dar es Salaam. info@tbs.go.tz, http://www.tbs.go.tz 255 (22) 2450206/2450949 Cell phone: 0782931197 (Gladness -TBS), 0786476284 (Jane-TPSF) kupata fomu ya kujisajili tafadhari tembelea, www.tbs.go.tz