Maonesho ya Viwanda vya Tanzania yatakayofanyika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es salaam

MAONESHO YA VIWANDA VYA TANZANIA YATAKAYOFANYIKA VIWANJA VYA MWL. J.K NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM.
Maonesho ya Viwanda vya Tanzania yaliyofanyika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es salaam
Wizara kwa kushirikiana na Tantrade inawaarika wananchi wote kufika bila bila kukosa katika maonesho ya Viwanda vya Tanzania, kuanzia tarehe 7 hadi tarehe 11 Disemba, 2017.
Katika maonesho hayo Viwanda na wajasiriamali mbalimbali wataonesha bidhaa mbalimbali wanazozalisha na kueleza shughuli wanazofanya katika uzalishaji wa bidhaa zao, ajira na teknolojia wanayotumia.
Hii itakuwa fursa nzuri kwa wananchi kujifunza na kupata chachu ya kuanzisha Viwanda na kujiajiri ili kufikia azma ya serikali ya Viwanda ifikapo mwaka 2025.
“TANZANIA SASA TUNAJENGA VIWANDA”