Mkutano Mkuu wa 22 wa umoja wa Mashirika ya Viwango Afrika ARSO unaofanyika jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Daudi Ntibenda alizungumza na wadau wa mashrikia ya viwango Barani afrika ambapo shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na shirika la viwango Afrika ARSO pamoja na wadau wengine kutoka mataifa ya ulaya na kufungua mkutano huo.
Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya wazalishaji wadogo wa bidhaa mbalimbali hapa nchini wanashindwa kufikia malengo ya kimataifa ya uzalishaji wa bidhaa zenye viwango bora kutokana na ukosefu wa elimu bora kulingana na soko la kimataifa.
Aidha endapo kama mashirika ambayo yanahusika na uratibu wa kuthamini viwango vya ubora watakuwa pamoja na wazalishaji hao ni wazi kuwa kiwango cha uzalishaji wa bidhaa zenye kiwango cha kimataifa utakuwa ni mkubwa.
Ntibenda alisema kuwa bado soko la uzalishaji wa bidhaa zenye kiwango linakabiliwa na changamoto nyingi sana na hivyo basi kuna umuhimu wa wadau wa viwango nchini kuhakikisha wanawatafuta na kujadiliana kwa pamoja namna ya kutafuta suluhu hizo ili kuweza kufikisha nchi kwenye kiwango cha kimataifa.
Alisisitiza kuwa kwa changamoto kubwa mojawapo ni pamoja na watengenezaji wa bidhaa kutengeneza bidhaa ambazo hazina viwango na hivyo kushusha nchi kwenye viwango vya kimataifa.
"kwa mfano kwa mji wa Arusha juzi tuu hapa mliweza kuona kuna mtu alikuwa anatengeneza saruji ambayo haina viwango lakini kwa kuwa mimi nilikuwa natambua umuhimu wa soko la kimataifa niliweza kumzuia"aliongeza Ntibenda
kutokana na hali hiyo aliwataka maafisa wa viwango hapa nchini kuhakikisha kuwa wananchana na tabia ya kukaa ofisisni na kisha kutaka wazalishaji wazalishe bidhaa zenye viwango vya kimataifa na badala yake waende mpaka viwandani kwa ajili ya kukagua na kuridhika hata kwa masoko ya nje ya nchi.
"nawashauri hata hawa TBS hakikisheni kuwa mnajiwekea utaratibuwa kuwafuata hawa wazalishaji wadogo na wa kati huko huko msibaki maofisini na kisha mkasema eti mnataka mshindane kimataifa kweli hamtaweza kabisa badala yake kila siku tutabaki na wimbo huu wa uazalishaji wa bidhaa zenye viwango vya kimataifa"aliongeza Ntibenda.
katika hatua nyingine Mkurugenzi mkuu wa TBS Tanzania, Bw. Joseph Masikitiko amesema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na mashirika mengine wamekutana jijini Arusha kwa malengo mbalimbali sanjari na kuwepo siku ya viwango Afrika.
Alimalizia kwa kusema kuwa wanatarajia kujadili mambo mbalimbali pamoja na maazimio ya pamoja na kupata njia muafaka za kupata bidhaa zinazolingana kwa viwango ili kuweza kupata bidhaa zinazotoka afrika zenye viwango sawa.