Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Mhe Charles Mwijage, akiwasilisha makadirio ya Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 Bungeni mjini Dodoma.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI AWASILISHA HOTUBA YA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 BUNGENI MJINI - DODOMA. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles J.P Mwijage (MB) awasilisha Hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 na kueleza vipaumbele na mikakati ya serikali ya awamu ya tano jinsi ilivyojipanga katika kuendeleza na kuinua Viwanda, Biashara, Masoko na Uwekezaji. Katika hotuba yake Waziri wa Viwanda amelieleza bunge kuhusu mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/2017 - 2020/21 ambao utekelezaji wake unaanza mwaka 2016/2017, Mpango huu unalenga katika kujenga uchumi wa viwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.