Habari
Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2025, fursa kwa wananchi na wafanyabiashara.
Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2025, fursa kwa wananchi na wafanyabiashara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesema kuwa, katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam, kutakuwa na siku maalumu ya michezo, ambapo Kombe la Klabu Bingwa Ligi Kuu Tanzania Bara litakuepo katika viwanja vya Tamasha hilo.
Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maonesho hayo, zikiwemo bidhaa na huduma mbalimbali katika viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba Juni 29, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Amesema, katika Tamasha hilo ambalo limeanza tarehe 28 hadi Julai 13, 2025 kutakua na huduma mbalimbali ambazo zitatolewa papo kwa hapo ikiwemo usajili wa Waandishi wa Habari kupitia Bodi ya Ithibati ya waandishi wa habari, usajili wa wasanii na elimu kwa wadau wa sanaa kupitia BASATA, kusajili jina la Biashara kupitia BRELA na huduma nyingi zinazopatikana katika viwanja hivyo vya maonesho.