Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

AfCFTA kukamilisha Kanuni za Uasili wa Bidhaa za Nguo na Mavazi


AfCFTA kukamilisha Kanuni za Uasili wa Bidhaa za Nguo na Mavazi

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jafo (Mb.) ametoa rai kwa Wataalamu wa Eneo huru la Biashara Afrika (AfCFTA)kuhakikisha majadiliano kuhusu Kanuni za Uasili wa Bidhaa za Nguo na Mavazi yanakamilika ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa nguo na mavazi kuzalisha kwa wingi na kupunguza uagizaji wa nguo na mavazi ikiwemo nguo zilizotumika.

Aidha amesisitiza kuendelea kuzihamasisha nchi sita (6) Barani Afrika zilizosalia kukamilisha mchakato na kuridhia mkataba huo ulioridhiwa na Nchi 48 ili kuharakisha utekelezaji wa Mkataba huo na kuchochea maendeleo ya uwekezaji, viwanda, biashara na kuimarisha uchumi ndani ya Afrika.

Waziri Jafo ameyasema hayo Aprili 15, 2025 wakati akihutubia katika Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la AfCFTA lililofanyika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) jijini Kinshasa ambapo Tanzania imekuwa mwenyekiti kwa mwaka 2024 na kukabidhi Uenyekiti huo kwa Misri 2025

Aidha katika kipindi hicho cha Uenyekiti, Waziri Jafo amebainisha kuwa AfCFTA imefanikiwa kukamilisha Kiambatisho cha Itifaki ya Uwekezaji cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji, Itifaki ya Biashara Mtandao, Kuridhia Kanuni za Mawaziri za kutoa upendeleo maalum wa soko kwa wafanyabiashara Wanawake na Vijana, Kuanzisha utaratibu wa mapitio ya utekelezaji wa Mkataba huo na Chombo cha  Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara.

Mpango wa kuhamasisha biashara ndani ya AfCFTA (GTI) unaotumiwa na Nchi Wanachama 39 umefanikiwa Kwa Tanzania hadi Januari 2025 imefanikiwa kuwa na Jumla ya Makampuni 43 ambayo imeweza kuuza bidhaa zake katika nchi mbalimbali za Afrika kupitia Mkataba huo kwa kutumia cheti cha uasili wa bidhaa cha AfCFTA ambapo, jumla ya vyeti 226 vimeweza kutolewa kwa Kampuni hizo. Bidhaa ambazo zimeuzwa kwa wingi kupitia vyeti hivyo ni nyuzi za katani tani 6,150 kwenda nchi za Nigeria, Ghana, Morocco na Misri; Vioo (Float Glasses) tani 1,433 kwenda Misri; Mchele tani 433 kwenda Burkina Faso na Cote d’ivoire; na kahawa tani 273.3 kwenda nchini Algeria.

Aidha, amebainisha kuwa AfCFTA imefanikiwa kuanzisha utaratibu wa kuwepo na Kampuni za Biashara (AfCFTA Trading Companies-ATC)