Habari
Makubaliano ya kuendelea na biashara kuanzia tarehe 02 Mei, 2025.
Picha mbalimbali zikionesha Majadiliano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi yaliyofanikisha makubaliano ya kuendelea na biashara kuanzia tarehe 02 Mei, 2025.
Tukio hilo muhimu limeongozwa na Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania na Mhe. Nancy Gladys Tembo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, tarehe 2 Mei 2025, jijini Dodoma.
Majadiliano hayo yamehusisha Mawaziri Hussein Bashe (Mb) wa Wizara ya Kilimo na Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb), wa Wizara ya Viwanda na Biashara za Tanzania; huku timu za wataalamu ziliongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Tanzania) na Wizara ya Viwanda na Biashara (Tanzania).
Kwa upande wa Tanzania, Makatibu Wakuu walikuwa Balozi Dkt. Samwel Shelukindo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Bw. Gerald Mweli wa Wizara ya Kilimo; na Dkt. Hashil T. Abdallah wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Tamko la Pamoja (Joint Communiqué) limesainiwa tarehe 2 Mei 2025 kufuatia kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje; Kilimo; Viwanda na Biashara wa pande zote jijini Dodoma.
Kusainiwa kwa Tamko la Pamoja ni uthibitisho wa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi kwa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo kulingana Mikataba na miongozo ya Kikanda na Kimataifa iliyopo.