Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Wasanii nchini waaswa kuwa mstari wa mbele katika uwekezaji pindi wanapopata mafanikio


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo( Mb) amewaasa wasanii nchini kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika uwekezaji pindi wanapopata mafanikio kwani nchi ina fursa kubwa ya uwekezaji.

Amesema wanapowekeza kwenye biashara itawasaidia pindi watapotoka kwenye tasnia ya sanaa au watapokuwa nje ya tasnia hiyo ili kujijenga kimaendeleo.

Ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Iftari iliyoambatana na Uzinduzi wa sabuni ya Wasafi Machi 20,2025 katika ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Da rs Salaam.

Aidha Dkt.Jafo amewaasa wasanii na Vijana kuendelea kushirikiana ma kusaidiana ili kusonga mbele na kuwahimiza kuendelea kupenda bidhaa za ndani kwani uwekezaji wa viwanda nchini umekuwa mkubwa sana hivyo kuna uwepo wa bidhaa nyingi zenye ubora na vilevile wapo vijana wengi wa Kitanzania wamewekeza hivyo kuendelea kuwaungq mkono kwa kujitoa kwako.

Vilevile Dkt.Jafo ameendelea kuhubiri amani kwa kuhakikisha Watanzania wote wanadumisha na kuilinda amani ua nchi kwani panapo amani ndioo kwenye maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wasafi Media Ndg.Nasib Abdul amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutengeneza fursa za uwekezaji nchini pamoja na kumshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) kwa ushirikiano wake na Wizara nzima katika kuunga mkono juhudi za uwekezaji wa viwanda na Biashara nchini.

Vilevile ametoa rai kwa vijana nchini kuchangamkia fursa nyungi zilizopo nchini hasa wakati huu wa uongozi wa awamu ya sita.