Habari
BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA VBU KUZUNGUMZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI
Balozi wa Uingereza nchini Bi. Diana Melrose leo amemtembelea Mhe. Waziri ofisini kwake. Balozi huyo ambaye aliongozana na maafisa kadhaa toka ofisi za Ubalozi amefanya ziara hiyo kwa lengo la kutoa salam za Mwaka Mpya na Pia kutoa hongera kwa Mhe. Waziri kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Viawanda, Biasharana Uwekezaji katika Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. John Pombe, Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe Balozi alielezea kuvutiwa na hali ya utulivu iliyopo nchini na kwamba nchi yake ingependa kuwekeza katika maeneo kadhaa ikiwemo usindikaji wa matunda na mbogamboga, gesi asilia na maeneo mengine ambayo nchi yake itaona inafaa. Kwa upande wake, Mhe. Waziri alifurahi kutembelewa na Balozi huyo na kumhakikishia ushirikiano wa kutosha katika kipindi hiki cha Uongozi wa Awamu ya Tano. Mhe Waziri amemkaribisha Mhe. Balozi na nchi yake kuwekeza kwenye usindikaji wa Samaki, mazao la kilimo kwa lengo la kuongeza thamani, usindikaji wa Korosho, ngozi na maeneo mengine ambayo Uingereza itakuwa tayari. Mhe. Waziri amemkaribisha Mhe Balozi kuja nchini na kuwekeza kwenye maeneo aliyoyataja kwa lengo la kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania ili baadae Tanzania iwe na uwezo wa kuuza bidhaa zilizosindikwa na kuongezwa thamani nje ya nchi badala ya ilivyo sasa ambapo bidhaa nyingi zinauzwa nje zikiwa ghafi. Mhe Waziri ameongeza kwa kusema, endapo suala hili litafanikiwa itakuwa imesaidia wakulima wetu kupata faida stahiki kupitia mazao wanayolima kwani umefika wakati sasa hata mkulima anapaswa kunufaika kwa kuuza mazao yao yakiwa yamesindikwa.