Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

CBE Yasisitizwa Kuwa Chachu ya Kuzalisha Wataalamu Mahir


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Said Msabimana amesema kuwa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) kinatakiwa kuwa chachu ya kutoa watendaji bora katika fani mbalimbali kwa ufanisi kwenye Taasisi na makampuni nchini.

Amebainisha hayo wakati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Hashili Abdallah katika Ufunguzi wa Kongamano la Fursa za Ajira na Maendeleo 2025 lililifanyikaka Kampasi Kuu ya Chuo hicho Jinini Dar es Salaam Juni 19,2025.

Bw. Msabimana amesema CBE ina jukumu la kuendelea kutoa Watendaji wenye ufanisi mzuri katika kada mbalimbali Nchini ambapo Chuo hicho kutoa wanafunzi wenye taaluma zinazolenga soko la Ajira nchini.

Aidha amesema anaamini kupitia Kongamano hilo vijana wataweza kupata uelewa mpana juu ya fursa za ajira, ujasiriamali na teknolojia ambapo hiyo ni hatua muhimu ya kujenga msingi wa ajira endelevu na maendeleo ya taifa la Tanzania.

Vilevile Bw. Msabimana amesititiza kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara itaendelea kushirikiana kwa karibu na CBE katika kuhakikisha vijana wanapata maarifa na stadi sahihi za kazi pamoja na ujasiri wa kujiajiri.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa CBE, Prof. Zacharia Mganilwa ameeleza kuwa kongamano hilo ni fursa ya pekee kwa wakufunzi kuangalia upya mitaala ili iweze kuendana na mahitaji halisi ya soko la ajira.

Naye Mkuu wa Chuo cha CBE, Prof. Edda Tandi Lwoga, amesema kuwa kutokana na tafiti iliyofanywa na Chuo hicho mwaka 2022 imegundua kuwa Wafanyakazi wengi waliopo kwenye Taasisi mbalimbali Nchini wametoka CBE kwani tafiti zinaonesha Asilimia 59 ya wahitimu wetu wameajiriwa, asilimia 20 wamejiajiri na asilimia 21 bado wanatafuta ajira.

Aidha Prof Lwoga amesema kuwa asilimia 96 ya wanafunzi wamethibitisha kuridhika na elimu waliyoipata CBE kutokana na kupatiwa mafunzo kwa nadharia na vitendo kwa kuzingatia uhitaji wa soko la ajira nchini.

Kongamano la Fursa za Ajira na Maendeleo 2025 limebeba kauli mbiu “Ubunifu na Ujasiriamali kwa Ajira Endelevu” likiwa na lengo la kuwaunganisha wanafunzi, waajiri, wahadhiri na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili mustakabali wa ajira nchin