Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

CHALAMILA AWAKARIBISHA WAGENI KATIKA KONGAMANO LA AFCFTA 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaaam, Albert Chalamila amewakaribisha na kuwahamasisha wageni kutoka nje ya nchi kujifunza lugha ya Kiswahili, wakati akitoa salam katika Kongamano la Afcfta la wanawake katika Biashara 2023 linalofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, 

"Tunayo furaha kuwapokea wageni wetu, karibuni wageni ili muweze kuwekeza katika nchi yetu, pia Tanzania tunatumia lugha ya Kiswahili tunaomba wageni hadi mtakapo ondoka muwe mmejifunza lugha yetu ya Kiswahili"

Kongamano hilo limeanza 6, December 2023 na litamalizika tarehe 8, Decemba 2023.