Habari
WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUZIFAHAMU SHERIA USHINDANI ILI KULINDA BIASHARA ZAO
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Bw. Sempeho Manongi, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, ametoa rai kwa wafanyabiashara na wadau wa soko nchini kuhakikisha wanazifahamu vyema sheria za ushindani ili kuepuka changamoto za kisheria zinazoweza kukwamisha biashara zao.
Bw. Manongi ameyasema hayo Machi 3, 2026 wakati akifungua semina ya Alisisitiza kuwa uelewa wa sheria hizo ndio ufunguo wa kulinda maslahi ya kila mshiriki wa soko na kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi. Alifafanua kuwa elimu inayotolewa na Baraza la Ushindani (FCT) si kwa ajili ya kutoa adhabu, bali ni kwa ajili ya kujenga mazingira bora ya biashara yanayozingatia uwazi, usawa, na ulinzi wa mlaji
Aidha, Bw. Manongi alibainisha kuwa Wizara inatambua soko huru na lenye ushindani wa haki kama nguzo kuu ya uchumi imara, na amewashauri wadau kutumia mifumo ya kisheria iliyopo pale wanapohisi kutendewa isivyo haki.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa FCT, Mhe. Jaji Rose A. Ebrahim, amwashauri wafanyabiashara kuepuka vitendo vya kupanga bei, kugawana masoko, au kuingia mikataba inayokandamiza ushindani na am. Alisisitiza kuwa kufanya biashara kwa uadilifu kunasaidia kupunguza gharama za maisha kwa wananchi na kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zinazotolewa sokoni.
Jaji Ebrahim aliongeza kuwa Baraza limeimarisha mifumo yake kwa kutumia TEHAMA na kuongeza uwazi katika utoaji wa maamuzi ili kuhakikisha rufaa zinashughulikiwa kwa haraka na kwa viwango vya kimataifa.
Naye Msajili wa Baraza la Ushindani (FCT), Bw. Wema Mbegu Kaskasi, alifafanua jukumu kuu la Baraza kuwa ni kusikiliza na kuamua rufaa zinazotokana na maamuzi ya mamlaka za udhibiti kama FCC, EWURA, LATRA, TCAA, TCRA, na PURA na kuwa semina hii ya Dar es Salaam ni mwendelezo wa mkakati wa kitaifa wa kupeleka elimu karibu na wadau, ambapo tayari wameshafika mikoa ya Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Mtwara, Lindi, na Dodoma.
