Habari
Changamkieno Fursa za masoko ya Kikanda na ya Kimataifa.

Changamkieno Fursa za masoko ya Kikanda na ya Kimataifa.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) amewaasa wahitimu wote waliomaliza katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuchangamkia fursa katika masoko ya Kikanda na Kimataifa ikiwemo Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) na Mpango wa Ukuaji na Fursa wa Afrika (AGOA).
Dkt.Jafo ameyasema hayo Novemba 21, 2024 katika mahafali ya 59 ya Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) huku yakiwa ya 40 kwa kampasi ya Dodoma yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kiketwe Convertion Centre jijini Dodoma.
Dkt. Jafo amewasisitiza kuwa wahitumu hao wanategemewa na Taifa kwa kuwa wamebobea katika taaluma zao hasa kwenye masomo ya Biashara,na amewataka kuwa chachu kwa kuchangamkia Biashara kwenye masoko mbalimbali yanayoizunguka Afrika katika Jumuiya za Kikanda na Kimataifa mbalimbali ambazo Tanzania ni Mwanachama.
"Leo hii kutokana na diplomasia nzuri chini Mhe Rais wetu amevutia uwekezaji ,ameweza kufungua masoko ya biashara kule china kwa kuruhusu bidhaa nyingi kuuzwa kule ikiwemo AGOA, ninyi wataalamu wa biashara tumieni fursa hiyo katika kupanua mtandao wa biashara ili Tanzania tuwe na viwanda vidogo vidogo vya kati na viwanda vikubwa" ,Amesema Mhe Jafo
Aidha , amekipongeza chuo Cha CBE kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali duniani unaosaidia kuwajengaa weledi vijana wanapomaliza vyuo na kuwapa maarifa ya kutosha ili kuhakikisha kwamba wanaifahamu vizuri dunia na kushiriki vizuri katika masuala ya kiuchumi ikiwemo Elimu mtandao.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof.Edda Tandi amesema kuwa Chuo hicho, kilichoanzishwa mwaka 1965 kina Wanafunzi 4438 wanasoma katika kozi mbalimbali katika kampasi ya Dodoma huku kikiwa na Programu 44.
Ameongeza kuwa Chuo Cha Elimu ya Biashara ndicho Chuo pekee nchini kinachotoa Elimu ya Vipimo na Viwango Basic (Metrology and stardzitaion) katika ngazi ya Astashada na Stashahada hivyo kuomba wazazi nchini kutumia nafasi hiyo kwa kuwapa nafasi watoto wao kusoma katika Chuo hicho.