Habari
Changamoto za Biashara Mtukula zitatatuliwa

Changamoto za Biashara Mtukula zitatatuliwa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeielekeza kuwa changamoto za Biashara katika Mpaka wa Mutukula zitatuliwe ili kurahisi
Maelekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deodatus Manyika (Mb) Novemba 22, 2023 wakati wa ziara ya Kamati hiyo ilipotembelea kituo cha pamoja cha forodha katika Mpaka wa Mutukula kwa lengo la kuangalia kwa utekelezaji wa kazi na majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia taasisi zake hususani Wakala wa Vipimo (WMA).
Mwanyika ameeleza kuwa wao kama Kamati kazi yao ni kuisimamia Serikali na kuishauri ili pale penye changamoto hatua zichukuluwe na pale penye mafanikio juhudi ziongezwe zaidi.
"Tumekuja kuangalia kwa ukaribu kama yale yanayotakiwa kufanyika yanafanyika kwa ufanisi pia katika ziara yetu tumebaini changamoto nyingi ,kubwa ikiwa ni ukosefu wa miundombinu ya kutendea kazi na upungufu wa wafanyakiazi" Alisema Mwanyika.
Aidha, amesema Kamati imebainia changamoto zote zinazofanya kuwe na mazingira magumu na kuisababishia Serikali kukosa mapato yake, kamati itashughurika nazo ndani ya Bunge na nje ya Bunge.
Kwa upande wake Naibu Waiziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe ( Mb) ameiahidi Kamati hiyo kuwa changamoto zote zilizoainishwa katika Kituo hicho Serikali itazitafutia ufumbuzi ikiwemo ukosefu watumishi na mashine ya kukagua mizigo (Cargo Scaner) kwa upande wa Tanzania.
"Sisi kama Serikali tunaowajibu wa kuboresha Mazingira ya Biashara Ili kuwe na uwezeshaji wa Biashara (Trade Facilitation) na utoaji wa huduma Ili magari yanayotoka upande wa Tanzania na upande wa jirani zetu Uganda yasipate vizuizi vya muda mrefu" Alisema Kigahe
Naye Mtendaji wa Forodha Kituo Cha Pamoja cha Biashara Mtukula ( OSBP) Bw. Steven Joseph Passange amewasilisha taarifa ya utendaji kwenye Kamati na kuainisha changamoto mbalimbali zinakikabili Kituo hicho ikiwemo ukosefu wa mashine ya kukagua mizigo( Cargo Scanner) hali inayosababisha wafanyabiashara kutumia muda mrefu kukagua mizigo yao na kutumia gharama kubwa kwa kuwalipa makuli kufanya kazi hizo.