Habari
Wawekezaji China kufungua Kiwanda cha Chokaa Visegese, Kisarawe ,Pwani.
Wawekezaji China kufungua Kiwanda cha Chokaa Visegese, Kisarawe ,Pwani.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo (Mb) amesema zaidi ya hekari 1,100 zimetengwa katika eneo la Visegese Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa ajili ya ujenzi wa viwanda mbalimbali.
Amebainisha hayo wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani humo, Machi 6, 2025 Dkt. Jafo amesema kuwa wawekezaji kutoka China wameahidi kuharakisha mchakato wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata chokaa ambacho kitakuwa cha kwanza kuanzishwa katika eneo hilo.
Aidha amesema kuwa eneo hilo la Visegese Wilayani humo ni eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda mbalimbali ambalo linaunganishwa na miundombinu ya barabara na msongo mkubwa wa umeme.
Dkt.Jafo ameongeza kuwa viwanda vingine vingi vitajengwa kwa lengo la kuongeza ajira kwa vijana na kutimiza adhma ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda nchini.