Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

ENDELEENI KUTOA ELIMU KWA VIJANA WAZITUMIE KATIKA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI-MHE.KIGAHE.


NDELEENI KUTOA ELIMU KWA VIJANA WAZITUMIE KATIKA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI-MHE.KIGAHE.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe(Mb) ameuagiza uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuendelea kutoa kozi ambazo wahitimu wanaenda kuzitumia moja kwa moja kwenye maisha ya kujiajiri na kuajiriwa pia.

Amebainisha hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Dkt. Selemani Jafo(Mb) katika Kongamano la Fursa za Ajira na Maendeleo 2025 lenye kauli mbiu “Ubunifu na Ujasiriamali kwa Ajira Endelevu” likiwa na lengo la kuwaunganisha wanafunzi, waajiri, wahadhiri na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili mustakabali wa ajira nchini lililofanyika Kampasi Kuu ya Chuo hicho Jijini Dar es Salaam Juni 20,2025.

Mhe.Kigahe amesema Uongozi na Wakufunzi wa Chuo hicho wanatakiwa kuendelea kuandaa mitaala na kuwafundisha juu ya ubunifu,kuwapa mawazo ya biashara kwa kika Mkoa kama wanavyofanya chuoni hapo ili kutoa wahitimu watakaoweza kujiajiri ili kuendana na mpango kazi wa Serikali ambao unahitaji kufikia asilimia 80 ya vijana wanaojiajiri mpaka kufikia 2030.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa CBE Prof. Zacharia Mganilwa amewaasa wanafunzi wasisome kwa ajili ya mitihani tu bali wasome kwa kuelewa na hio itawafanya kuwa wabunifu wakubwa kwasababu elimu inawapa maarifa mbalimbali pamoja na Kupitia maboresho ya mitaala Chuo hicho kitaongeza programu zinazoendana na soko la ajira na kuwaandaa wahitimu kitaaluma, kivitendo na kimaadili.

Naye Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE Prof. Edda Tandi Lwoga amesema kuwa Kongamano hilo linaunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza na kufundisha mitaala kwa vitendo na programu ya atamizi (incubation) ambayo inahamasisha wanafunzi wenye ndoto za biashara au bunifu zao kuzilea mpaka wanapokuwa wafanyabiashara kamili ili kupunguza pengo kati elimu na mahitaji ya soko la ajira.

Aidha Prof. Lwoga amesema kuwa CBE inajivunia kuwa na wataaluma wenye vigezo ambao wamesoma ndani na nje ya nchi ambao wanaweza kutoa elimu sahihi kwa wanachuo ili kuzalisha vijana wenye utendaji wa hali ya juu kuendana na kasi ya kujiajiri na kuajiriwa