Habari
NAIBU WAZIRI LONDO AWASILI UTURUKI KUSHIRIKI TAMASHA LA TEKNOFEST 2026.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, amewasili nchini Uturuki kwa ajili ya kushiriki Tamasha la 15 la Anga na Teknolojia (TEKNOFEST), linalofanyika katika mji wa Şanlıurfa kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 4, 2026.
Mhe. Londo amepokelewa Septemba 30, 2026 na Sadık Çiçekli Mkuu wa Idara ya Mahusiano, pamoja na Cemal Yüksel anayeshughulikia Itifaki kutoka Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Uturuki.
Aidha Naibu Waziri Londo anashiriki tamasha hilo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith S. Kapinga (Mb.), ambaye alialikwa na Waziri wa Viwanda na Teknolojia wa Uturuki, Mhe. Mehmet Fatih Kacır, kushiriki TEKNOFEST.
Kwa mujibu wa barua ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Septemba 9, 2026, imeeleza kuwa TEKNOFEST ni jukwaa la kimataifa linalowakutanisha wataalamu wa teknolojia, viongozi wa sekta za viwanda na teknolojia, watunga sera, vijana pamoja na wadau kutoka sekta za umma na binafsi.
Tamasha Hilo linalenga kuonesha muhimu wa teknolojia, Ubunifu na ANGA katika Sekta ya Viwanda na sayansi kwenye maendeleo ya teknolojia na Uvumbuzi
