Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

MHE LONDO ASHIRIKI KIKO CHA VIONGOZI NA WATAALAMU WA AFRIKA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA BIASHARA NA   UWEKEZAJI


 📌Ashiriki mjadala wa kitaalamu ngazi ya  wa Mawaziri kujadili fursa na vipaunbele vya kisera kwa Afrika;

📌 Namibia yaonesha nia ya uwekezaji Tanzania kwenye sekta za mifugo, miundombinu na mazao ya kilimo.

WINDHOEK, NAMIBIA

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe Dennis Londo yuko nchini Namibia kushiriki kikao cha pamoja cha kamati ya wakuu wa viongozi na wataalamu wa Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika kujadili fursa za biashara na uwekezaji.

Mkutano huo wa pamoja una lengo la kujadili namna ya kuunganisha Afrika Mashariki na kusini kwenye nyanja za miundombinu unganishi, biashara na uwekezaji ambapo Mhe Londo alipata nafasi ya kunadi fursa za uwekezaji Tanzania.

Akiwa kwenya mjadala wa kitaalamu ngazi ya Mawaziri Mhe Londo amesema kuwa nchi ya Namibia na Tanzania zina makubaliano ya ushirikiano kwenye  sekta za biashara, uwekezaji na viwanda kwa ujumla hivyo ni vema kutumia masoko ya kikanda kuuza bidhaa zake.

Aidha, amesisitiza pia umuhimu wa kutumia fursa zilizopo katika sekta za madini, mafuta ya petroli, mifugo, utalii na uvuvi kukuza uchumi na kusisitiza pia kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji walioonesha Nia ya uwekezaji kupatiwa fursa hizo hususani kwenye sekta za mifugo na kusisitiza pia  umuhimu wa kushughulikia vikwazo visivyo vya kikodi (NTBs) vinavyoathiri bidhaa za Tanzania katika soko la Namibia na kuwaunganisha wadau wa biashara ili kurahisisha upatikanaji wa masoko. 

Mkutano huo umeandaliwa ma tume ya uchumi ya umoja wa mataifa kwa Afrika-UNECA kwa kushirikiana na kanda ya Afrika Mashariki -SRO-EA