Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

NAIBU WAZIRI LONDO ASHIRIKI KILELE CHA TAMASHA LA TEKNOLOJIA UTURUKI.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo ameshiriki Tamasha la  Anga na Teknolojia (TEKNOFEST) lililofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Şanlıurfa GAP, nchini Uturuki, kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 4, 2026. 

Ushiriki huo umefanyika kufuatia mwaliko wa Serikali ya Uturuki kupitia Wizara ya Viwanda na Teknolojia, huku tamasha hilo likihusisha wataalamu, vijana na wadau mbalimbali katika kuonesha maendeleo ya sayansi, teknolojia, ubunifu na anga. 

Tamasha hilo limefikia kilele Oktoba 03 kwa hafla ya kufunga na utoaji wa tuzo, iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Türkiye, Recep Tayyip Erdoğan, likiwa ni moja ya majukwaa makubwa yanayowakutanisha wadau wa viwanda teknolojia, ubunifu na maendeleo ya kisayansi.