Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mazungumzo kati ya Waziri Jafo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bwana Andrew Lentz


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Selemani Jafo(Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bw.Andrew Lentz, Aprili 08,2025 katika ofisi ya Wizara Jijini Dodoma.

Aidha mazungumzo hayo yamelenga katika Kuimarisha ushirikiano wa Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Marekani, Kuendeleza majadiliano ya Biashara (commercial dialogue) baina ya nchi hizo pamoja na Mpango wa AGOA na mustakabali wa sera mpya ya Biashara ya Marekani kwenye ushuru wa Bidhaa zinazoingia nchini humo.