Habari
DKT. ABDALAH: SERIKALI NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA KUKUTANA KILA MWEZI

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imeweka mikakati ya kukutana na Jumuiya ya wafanyabishara Tanzania kila mwezi ili kujadili masuala mazima yatakayohusisha sera za kibiashara nchini.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi mpya wa Jumuiya hiyo Desemba 27,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Cate Hotel Dar es Salaam.
Aidha amebainisha kuwa katika kukutana baina ya Serikali na Jumuiya hiyo Taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za Wizara hiyo zinazohusika na Biashara pamoja na zile za nje ya Wizara hiyo ambazo zinahisuka moja kwa moja katika kuhudumia biashara nchini.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Ghalib Said Mohamed ametoa pongezi kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara na Jumuiya hiyo pia ameeleza kuwa kikao kazi hicho kitaongeza chachu ya uboreshaji hali ya Biashara nchini.