Habari
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) atoa wito kwa wanawake wa Tanzania kushiriki Kongamano la Pili la Wanawake katika Biashara chini

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ametoa wito kwa wanawake wa Tanzania kushiriki Kongamano la Pili la Wanawake katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika ( AfCFTA) litakalofanyika Disemba 06 - 08, 2023 katika JNICC Dar es Salaam kwa kujisajili kupitia anuani ya Tovuti i www.viwanda.go.tz
Ameyasema Novemba 29, 2023 akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hashil Abdallah alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusu Kongamano hilo linaloongozwa na Kauli Mbiu "Kuimarisha Ushiriki wa Wanawake katika Biashara na Kuongeza Kasi ya Utekelezaji wa AfCFTA” ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.
Vilevile, Amebainisha kuwa Kongamano hilo linalenga kuwakutanisha pamoja wanawake katika biashara waweze kujadiliana, kubadilishana uzoefu, kutatua changamoto wanazokabiliana nazo na kuweka mikakati ya kuimarisha ushiriki wao kwenye biashara ndani ya Afrika chini ya AfCFTA ili kuongeza ajira na kukuza uchumi imara kwa Taifa
Aidha amesema washiriki wapatao 700 wanatarajiwa kushiriki Kongamano hilo wakiwemo Viongozi mbalimbali wanawake kutoka ndani na Nje ya Afrika katika ngazi ya Marais, Marais Wastaafu, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Kimataifa, Watu Mashuhuri, Mawaziri wa biashara na masuala ya jinsia na wanawake na wafanyabiashara pamoja na maonesho ya wafanyabiashara wanawake kutoka katika nchi 55 za Afrika.
Aidha, amesema, Kongamano hili la Wanawake katika Biashara la AfCFTA, ni Kongamano la pili kufanyika ambapo Kongamano la Kwanza lililofanyika 12-14 Septemba 2022 Dar es Salaam na lilifanikiwa kukamilisha Rasimu ya Itifaki ya Wanawake na Vijana katika Biashara ndani ya AfCFTA
Aidha, Dkt. Kijaji amesema Kampuni 18 zinazofanya biashara ya kuuza bidhaa katika soko la AfCFTA yakiwemo makampuni ya wanawake ya ANISIA Group (Tanzania) linalouza bidhaa za karafuu Morocco na AJA (T) Ltd linalouza Kamba za katani Ghana.