Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt.Hashil Abdallah ametoa rai kwa wataalamu wa mauzo nchini kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya mauzo Duniani.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah ametoa rai kwa wataalamu wa mauzo nchini kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya mauzo Duniani.

Ametoa rai hiyo wakati akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) kufungua Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mauzo kutoka sekta binafsi na Serikalini uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Protea e Dar es Salaam Nov 22,2024.

Dkt.Abdalah amesema kwa sasa teknolojia ya mauzo Duniani imebadilika sio kama hapo awali kwani kumekuwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa hivyo haiwezekani tena kutegemea uuzaji wa njia za zamani kwani Mazingira ya kisasa ya mauzo yanadai kuchukua njia, mikakati na mawazo mapya.

Aidha Dkt.Abdallah amesema Mkutano huo ukawe moja ya jukwaa la kubasilishiana mawazo na ujuzi kwa wataalamu hao ambapo utachagiza uchumi wa nchi kwani hadi sasa Taifa la Tanzania limepiga hatua kubwa katika maendeleo ya miundombinu, uvumbuzi wa biashara, na ukuaji wa uchumi na pia Soko la Afrika Mashariki linazidi kuwa kitovu cha biashara za kimataifa hivyo kama wataalamu wa mauzo ni fursa kwao.

Nae Mratibu wa Mkutano huo Bi. Fatma Mnaro amesema pamoja na Mkutano huo pia kumezinduliwa Kituo cha Mauzo (Sales Hub Tanzania) ambacho kimeundwa kuleta mapinduzi katika tasnia ya mauzo wakiwemo Wakurugenzi,mameneja na Maafisa nchini Tanzania ili kuunda jumuiya mahiri kwa wataalamu wa mauzo kuungana, kushirikiana na kuboresha ujuzi na uwezo wao katika tasnia ya mauzo pamoja na kuzindua Mpango wa Wanawake katika Mauzo Tanzania ili kuwawezesha na kuwaunganisha wafanyabiashara wa kike, wenye shauku ya kufanya mauzo nchini.