Habari
Dkt. Hashil .Abdallahakishiriki Mkutano wa 16 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC)
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallahakishiriki Mkutano wa 16 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda 26 Julai 2025,
Mkutano huo ulihusisha utiaji saini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano ikiwemo ya kilimo na uanzishwaji wa Ofisi ya Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) jijini Kigali, kama sehemu ya hatua za kuimarisha uhusiano wa karibu na kukuza maendeleo ya pamoja baina ya nchi hizo mbili.
Hati hizo zimesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Olivier Nduhungirehe ikilenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Rwanda kwa manufaa ya wananchi wa mataifa haya mawili.
Kupitia makubaliano ya sekta ya kilimo, pande zote zimekusudia kubadilishana uzoetu, teknolojia, utaalamu na tarifa muhimu ili kuongeza uzalishaji, usalama wa chakula na fursa za biashara ya mazao ya kilimo.