Habari
Dkt Jafo azikataa taasisi kuendela kusaidia uwekezaji viwandani.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) ameziagiza taasisi wezeshi katika viwanda kuendelea kutoa huduma kusaidia shughuli za viwandani.
Ameyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kutembelea viwanda vya kuzalisha Mifuko cha Future Colourful Ltd na Kiwanda cha viatu cha Jinkui Ltd vilivyopo Zuzu Mkoani Dodoma Januari 14,2025.
Dkt.Jafo amesema taasisi wezeshi ziendelee kuhakikisha upatikanaji wa huduma kama vile maji ili viwanda hivyo visisimame kufanya kazi ili kusaidia vijana wanaopata ajira viwandani kuendelea kufanya kazi kupungiza ukosefu wa ajira.
Aidha Dkt.Jafo amezitaka taasisi za usimamizi wa uwekezaji Viwandani kuhakikisha zinakuwa na malengo za kuwasaidia wawekezaji na si wakwamishaji kwenye suala la uwekezaji na shughuli za viwandani.
Dkt.Jafo pia ameendelea kuwahamasisha Watanzania nchini kuendelea na desturi ya kutumia bidhaa za ndani ili kuzipa thamani na kupata masoko.