Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt.Selemani Jafo (Mb) amewashauri Wamiliki wa Matipa na Mitambo Nchini (TTMOA) kuanzisha kampuni kubwa ya Kandarasi yenye misingi ya kiuchumi


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) amewashauri Wamiliki wa Matipa na Mitambo Nchini (TTMOA) kuanzisha kampuni kubwa ya Kandarasi yenye misingi ya kiuchumi ambayo itaweza kuwekwa kwenye soko la hisa na kufanya kuwa kampuni kubwa zaidi ambayo itaweza kuchukua kazi za Miradi mikubwa Nchini.

Ameyasema hayo wakati anafungua Mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wamiliki wa matipa na mitambo Tanzania (TTMOA) 2024 uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip ,Masaki Jijini Dar es Salaam Novemba 20,2024

Waziri Jafo amesema endapo Umoja huo utaweza kuanzisha Kampuni hizo basi utaweza kuwa na nafasi kubwa kama wazawa kupewa miradi mbalimbali.

Aidha Dkt. Jafo amewaahidi wamiliki hao kuwa atashirikiana na Wizara za kisekta kutatua changamoto zao ikiwemo kupewa miradi ambayo wazawa wanaweza kuifanya kwani kumekuwa na changamoto ya wageni kufanya shughuli ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya pia ili kuwafanya Watanzania kuwa na uchumi ili kuendana na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanznia Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Vile vile Dkt.Jafo amewataka Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa endapo wanaandaa michakato ya kutoa maeneo ya kuchimba vifusi na madini ujenzi mengine wawaangalie Watanzania kwani sekta hiyo inawagusa Watanzania moja kwa moja na inatoa kiasi kikubwa cha ajira kwa Watanzania.

Nae Mwenyekiti wa taasisi hiyo ya TTMOA Ndg Emmanuel Moshi ameishukuru Serikali kwa kuona haja ya kulinda wazawa na wafanyabiashara wa ndani ili kuwa sehemu ya ujenzi wa miradi na kuwezeshwa kwenye uwekezaji wa miradi