Habari
Dkt. Hashil T. Abdallah ameingoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Kikao cha Makatibu Wakuu Julai 24, .2025 Jijini Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah ameingoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Kikao cha Makatibu Wakuu Julai 24, .2025 Jijini Arusha kikitangulia Mkutano Maalum wa Kisekta wa Mawaziri wa Fedha na Mipango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kitakachofanyika Julia 25,2025.
Mkutano huo unalenga kujadili suala la ushuru baguzi wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya EAC kinyume na Ibara ya 15 ya Itifaki ya Umoja wa Forodha wa EAC na hatua za kikodi zilizopo kwenye sheria za fedha za mwaka 2025/2026 zenye athari hasi kwa biashara ya kikanda, na kupendekeza marekebisho yatakayowezesha utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Forodha na Itifaki ya Soko la Pamoja la EAC
Lengo la Mkutano wa Kwanza wa Dharula wa SCFEA ni kupokea na kujadili utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Mkutano wa 46 wa Baraza la Kisekta la EAC la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI), Mkutano wa 17 wa SCFEA pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Mashauriano ya Kibajeti iliyofanyika mwezi Mei 2025.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu ulioongozwa na Dkt,Abdallah akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya fedha pamoja na wawakilishi wa Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Watalaam kutoka Afisi ya Rais – Fedha na Mipango Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Sukari Tanzania.