Habari
Dkt. Hashil Twaibu Abdallah ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Twaibu Abdallah ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu Jijini Antananarivo Madagascar kwenye Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Agosti 10, 2025.Mkutano Ngazi ya Mawaziri unafanyika Agosti 12 hadi 14, 2025.
Aidha, Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali unafanyika Agosti16 hadi 17, 2025 nchini humo.
Mkutano huu ulianza Agosti 4, 2025 na unatalajiwa kuhitimishwa Agosti 17, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Ivato Jijini Antananarivo - Madagascar