Habari
DKT.JAFO - SERIKALI HAIJAZUIA WAGENI KUFANYA BIASHARA BALI WAFUATE TARATIBU ZETU.
DKT.JAFO - SERIKALI HAIJAZUIA WAGENI KUFANYA BIASHARA BALI WAFUATE TARATIBU ZETU.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali ya Tanzania haijazuia Wafanyabishara na wawekezaji kuja kufanya biashara Tanzania bali imelenga kila kitu kifanyike kwa utaratibu kama ilivyo katika nchi nyingine ili kulinda maslahi ya Watanzania.
Amebainisha hayo katika Kongamano la Biashara la Kariakoo (Kariakoo Festival 2025) likiwa na lengo la kuunganisha Wafanyabishara, taasisi za umma, watoa huduma na maelfu ya wateja kutoka ndani na nje ya nchi, tukik lililofanyika Agosti 15,2025 Katika Soko la Kariakoo Jijini Dar es salaam.
Waziri Jafo amesema serikali iliweka mikakati kadhaa ya kuhakikisha shughuli zinazotakiwa kufanywa na watanzania zifanywe na watanzania na kusisitiza kuwa utaratibu wote ulifanywa kwa ushirikiano kati ya Wafanyabishara na serikali.
Aidha Waziri Jafo amewaasa Wafanyabiashara hao kutumia soko jipya la Kariakoo vizuri na wana kila sababu ya kulinda soko hilo kwani Serikali imewekeza fedha nyingi na pia ndio soko linaloleta heshima kwa wafanyabiashara nchini.
Vile vile Dkt.Jafo amewaasa Wafanyabiashara hao wa Kariakoo kutumia Tamasha hilo kuzitumia taasisi za Serikali zilizopo hapo kutatua changamoto zao za kibiashara.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo amemshukuru kamishna wa TRA kwa kuweka utaratibu bora wa ukusanyaji wa kodi jambo ambalo linaongeza mapato ya serikali.
Kwa Upande wake Kamishna mkuu wa TRA Bw. Yusuph Mwenda amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Wafanyabishara nchini katika mambo yote ikiwa ni pamoja na punguzo la kodi kwani kuanzia mwezi ujao Wafanyabishara wote watakaolipwa kodi kidigitali kutakuwa na punguzo kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 16