Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

DKT.JAFO AITAKA FCT KUHARAKISHA MASHAURI 32 ILI KUKUZA BIASHARA NA KUONDOA VIKWAZO


DKT.JAFO AITAKA FCT KUHARAKISHA MASHAURI 32 ILI KUKUZA BIASHARA NA KUONDOA VIKWAZO

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amelitaka Baraza la Ushindani kushughulikia kwa haraka mashauri 32 yanayosubiri usuluhishi ili kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara na kuimarisha ushindani wa haki sokoni.

Amebainisha hayo wakati wa Uzinduzi wa Baraza jipya la Ushindani Jijini Dar es Salaam Julai 18,2025 ambapo Dkt. Jafo alieleza kuwa tangu Juni mwaka jana, Baraza halikuwa na wajumbe, hali iliyosababisha mashauri mengi kubaki bila mwelekeo.

Dkt Jafo alitoa ametoa rai kwa Baraza hilo kuepuka vitendo vya rushwa na kuhakikisha kuwa maamuzi ya Baraza yanazingatia misingi ya haki na ushindani wa kweli na kuwa waangalifu na kutoa maamuzi kwa mujibu wa sheria kwani Taasisi hiyo ni huru na hakuna mtu atakayeingilia kazi yao.

Nae Mwenyekiti wa Baraza hilo Jaji Rose Ibrahim amesema kama Baraza wamepanga kuyashughulikia mashauri yote kwa haki, bila upendeleo na kwa kasi inayostahili ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake, Msajili wa Tume ya Ushindani (FCT), Bw. Mbegu Kasikasi, alieleza kuwa mashauri 32 yaliyopo ni ya aina mbalimbali, yakiwemo yale yanayohusiana na sekta za nishati, maji na umeme chini ya mamlaka kama vile EWURA, pamoja na masuala ya bidhaa feki yaliyowasikishwa na Tume ya Ushindani (FCC).

Bw.Kaskasi amesema Tangu Juni hakukuwa na Baraza wala wajumbe hivyo Mashauri mengi yako katika hatua tofauti na sasa wamewezesha mfumo wa kielektroniki kusaidia upatikanaji wa haki kwa haraka.

Uzinduzi huu unafanyika wakati ambao dira mpya ya maendeleo ya viwanda na biashara, iliyozinduliwa jana na Rais Samia Suluhi Hassan, ikiweka matarajio makubwa kwa taasisi za udhibiti kusaidia kuleta kasi ya ukuaji wa uchumi na kushughulikia changamoto kama bidhaa bandia.