Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

ELSEWEDY CHAAAGIZWA KUENDELEA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekiagiza Kiwanda cha Elsewedy Electric Industrial Cable kuendelea kuzingatia ubora wa bidhaa zao ili kulinda uaminifu katika soko la kimataifa kwa maslahi ya uchumi wa Tanzania.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya kiwanda hicho kilichopo Kigamboni Jijini Dar es salaam Agosti 26,2025.

Waziri Jafo amesema Kiwanda hicho kinazalisha tani 1100 kwa mwezi na kati ya hizo tani mia tano 500 ni shaba na Aluminiam ni zaidi ya tani mita sita 600 ambazo zinauzwa katika nchi mbalimbali kama Kenya, Sudan, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia na nchi nyingine hivyo Tanzania inaenda kujitosheleza kwa mahitaji ya ndani.

Aidha waziri Jafo amefurahishwa na vijana wa kitanzania kurithishwa teknolojia ya kisasa inayotumika katika kiwanda hicho jambo ambalo limewezesha vijana wengi kupata ajira katika kiwanda hicho.

Vilevile Dkt. Jafo ameziagiza taasisi wezeshi kusaidia Viwanda kama hivyo ili kuhakikisha vinaendelea kuzalisha bidhaa za kutosha.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Mhandisi Ibrahim Qamar ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono uwekezaji na kubainisha kuwa wana mpango wa upanuzi wa kiwanda hicho ili kufikia nchi nyingi huku lengo kubwa likiwa ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu chao.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bi.Pendo Mahalu amekaribisha makampuni mengine yenye nia njema kuwekeza Kigamboni kwani wana eneo kubwa linalofaa kwa ajili ya uwekezaji.