Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

MAONESHO YA EXPO 2025 OSAKA JAPAN, KULETA SURA MPYA YA MAENDELEO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI TANZANIA.


The Minister of Industry and Trade, Hon. Dr. Selemani Jafo, has called upon business stakeholders in the country to seize the business opportunities at the World Trade Exhibition EXPO 2025 OSAKA, JAPAN. Through this global exhibition, Tanzanians will have the opportunity to meet with various stakeholders in the sectors of Tourism, Infrastructure, Arts, Science and Technology, Agriculture, Livestock, Fisheries and the Blue Economy, Health, Kiswahili Language and Culture, Energy, and Investment.

Furthermore, Minister Jafo urged Tanzanians to register in greater numbers through the Tanzania Trade Development Authority (TanTrade) website, which is www.tantrade.go.tz, to increase the number of participants from Tanzania in the exhibition in Japan. This World Trade Exhibition EXPO 2025 Osaka Japan is being coordinated by TanTrade in collaboration with the Tanzanian Embassy in Japan. This information was revealed today at a press conference held at the Airports Authority meeting hall, Terminal I, in Dar es Salaam.



Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jafo ametoa rai kwa wadau wa biashara nchini, kuchangamkia fursa za kibiashara kwenye maonesho ya Biashara ya Dunia EXPO 2025 OSAKA, JAPAN. Kupitia maonesho hayo ya dunia Watanzania watapata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali katika sekta za Utalii, Miundombinu, Sanaa, Sayansi na Teknolojia, Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Afya, Lugha ya Kiswahili na Utamaduni, Nishati, na Uwekezaji.

Aidha Waziri Jafo amewasisitiza Watanzania kujisajili kwa wingi zaidi kupitia tovuti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade ambayo ni www.tantrade.go.tz ili kuongeza idadi ya washiriki kutoka Tanzania kwenye Maonesho hayo nchini Japan, Maonesho haya ya Biashara ya Dunia EXPO 2025 Osaka Japan yanayoratibiwa na TanTrade kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan. Maelezo haya yamebainishwa leo katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Terminal I, Jijini Dar es Salaam.