Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Baraza la Ushindani (FCT) kuhakikisha kuwa linaendelea kufanya kazi kwa weledi,


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) amelielekeza Baraza la Ushindani (FCT) kuhakikisha kuwa linaendelea kufanya kazi kwa weledi, upendo na ushirikiano ili kuwapa Wawekezaji na Wafanyabiashara uhakika wa usalama wa mitaji yao na kuongeza wawekezaji nchini.

Dkt. Jafo ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma alipotembelea Baraza hilo Aprili 24, 2025, ambapo ameeleza kuwa kama Wizara ina jukumu la kuhakikisha taasisi zote zilizo chini yake zinafanya kazi kwa bidii na kuwasaidia watanzania.

Aidha , amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha inaweka mazingira rafiki na wezeshi ya ushindani wa haki katika biashara na utoaji huduma na kuzitaka mamlaka za udhibiti kutekeleza azma hiyo ya serikali.

Kwa upande wake, Msajili wa FCT Bw. Wema Mbegu Kaskas, ameeleza kuwa FCT inatekeleza jukumu la kusikiliza rufaa na mashauri yanayotokana na mamlaka mbalimbali za udhibiti hapa nchini.

“Baraza hili limeweza kuamua mashauri 460 hadi sasa tangu lilipoanzishwa 2007 na linaundwa na wajumbe sita pamoja na mwenyekiti ambaye huteuliwa kutoka miongoni mwa majaji wa Mahakama Kuu, na wote ni wateule wa Rais,” alisema Wema.

Aidha, amebainisha kuwa mtu yeyote ambaye hataridhishwa na maamuzi ya Mamlaka za udhibiti kama " Mamlaka ya udhibiti wa sekta ya maji (EWURA), Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa anga (TCCA), Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini (LATRA), Mamlaka ya udhibiti wa huduma za mawasiliano (TCRA) na Mamlaka ya udhibiti wa mkondo wa juu wa Petroli (PURA)," anaweza kuwasilisha rufaa yake FCT.

Aliongeza kuwa kwa sasa wameanzisha mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kupokea na kuhifadhi mashauri hayo, ili kuboresha huduma