Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

serikali itaendelea kuvilinda viwanda vya ndani.


Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani jafo(Mb) amesema serikali itaendelea kuvilinda viwanda vya ndani dhidi ya bidhaa zinazotoka nje zilizo chini ya viwango vya ubora na kuuzwa kwa bei rahisi lengo likiwa ni kusaidia kukua kwa uchumi wa nchi unaoleta ustawi wa viwanda.

Amebainisha hayo wakati akizindua kiwanda cha mabati ya rangi cha ALAF uliogharimu zaidi ya dola milioni 25 za kimarekani Juni 03,2025 Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Jafo amesema Mkakati wa Serikali ni kuwezesha mradi wa chuma wa Liganga na Mchuchuma pamoja na mradi wa Maganga Matitu kufanya kazi kwa ufanisi ili kuwezesha viwanda kuacha kuagiza malghafi za chuma kutoka nje ili kuwezesha viwanda vya ndani na kutumia malghafi za ndani katika uzalishaji wa bidhaa ikiwemo mabati.

Mtambo huo wa uzalishaji wa mabati ya rangi unauwezo wa kuzalisha tani elfu 75 za mabati ya rangi kwa mwaka ni asilimia 50 ya mahitaji ya soko ambapo yanakadiliwa kuwa tani 130,000 kwa mwaka.