Habari
SERIKALI KUJA NA MKAKATI WA KUFUFUA KIWANDA CHA EAST AFRICAN CABLES

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt Selemani Jafo (Mb) amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuja na mkakati wa kufufua Kiwanda cha East African Cables ambacho shughuli zake za uzalishaji zimekuwa hazifanyi vizuri.
Amebainisha hayo wakati wa ziara yake katika Kiwanda hicho kinachozalisha nyaya za umeme kilichopo eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2025
Waziri Jafo amesema kiwanda hicho ambacho Serikali ina hisa 29% ,East African Cables 51%, 10% TANESCO, na 10% Fedha za Maendeleo Tanzania hivyo Serikali ina kazi ya kukiwezesha kiwanda hicho ili kulinda ajira za Watanzania na historia nzuri ya Tanzania juu ya kiwanda hicho.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Bw.Geoffrey Odhiambo ameiomba serikali kuweka mkono wake katika kiwanda hicho ili kuongeza uzalishaji na kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi katika kiwanda hicho.