Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika Kongani ya Viwanda ya Kwala, mkoani Pwani,


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika Kongani ya Viwanda ya Kwala, mkoani Pwani, tayari viwanda saba vinafanya kazi huku vingine vitano vikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi.

Kongani hiyo yenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 3 imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 2,500, na inalenga kuwa na zaidi ya viwanda 200, hatua inayotarajiwa kuimarisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya viwanda nchini.Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo Julai 29, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Mhe. Jafo amesema kuwa uwekaji wa jiwe la msingi unakwenda sambamba na uzinduzi wa treni ya mizigo pamoja na bandari kavu, hatua inayokusudia kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa kwenda masoko ya ndani na nje ya nchi.

Aidha, ameeleza kuwa viwanda hivyo vinajihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo vifaa vya ujenzi, vilainishi vya magari, betri, nguo, friji na vipodozi.
Kwa mujibu wa Waziri Jafo, mradi huo mkubwa unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 50,000 za moja kwa moja na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 150,000 kwa Watanzania, ambapo tayari watu 311 wamekwishapata ajira kupitia shughuli zinazoendelea katika eneo hilo.

“Kipindi cha mwaka mmoja ujao, tunatarajia kuongeza ajira za moja kwa moja 1,300 na ajira zisizo za moja kwa moja 700,” alisema.

Hadi sasa, kiasi cha Dola milioni 30 kimetumika katika uwekezaji wa kongani hiyo, na mapato kuwa Dola milioni 31 kwa mwaka kutokana na viwanda vinavyofanya kazi kwa sasa.

Dkt Jafo alisema mradi huo unalenga kuwa kitovu cha uhawilishaji wa teknolojia kwa kuchakata malighafi za Tanzania na kuongeza thamani kabla ya kuziuza kwenye masoko ya kimataifa, hivyo kukuza uchumi wa taifa kwa njia endelevu.
Aidha, Waziri huyo alieleza kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji yameandaliwa katika Kongani ya Kwala, ikiwa ni pamoja na miundombinu bora ya barabara, umeme, maji, mawasiliano, na huduma za kijamii, huku maboresho zaidi yakiendelea kufanyika.

Akizungumzia mwelekeo wa maendeleo ya viwanda mkoani Pwani, Dkt Jafo alisema mkoa huo umeendelea kung’ara katika sekta ya viwanda