Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt.Selemani Jafo amewaasa Watanzania kuendelea kutunza amani ya nchi kwa kuhakikisha wanaepukana na vitendo vitakavyovunja amani


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo amewaasa Watanzania kuendelea kutunza amani ya nchi kwa kuhakikisha wanaepukana na vitendo vitakavyovunja amani hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Dkt.Jafo amesema amani iliyopo nchini ni ya muhimu na haina budi kulindwa ili Taifa liendele kupiga hatua kwani nchi inapochafuka hata maendeleo huduma.

Amebainisha hayo wakati alipokuwa Mgenineasmi katika Mashindano ya 11 ya kuhifadhi Quran tukufu Nyanda za kusini Machi 23,2025

Dkt.Jafo amewaasa Wazazi kuhakikisha wanawaandaa vizuri watoto vizuri kwa kuwapatia elimu za dini ili wawe na maadili mema hasa katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi wa Ramadhan na Kwaresma.

Aidha ametoa ushauri kwa kamati za mashindano ya Quran kuhakikisha kunakuwa na zawadi kwa walimu ambao bijana wao wanashinda ili kuendelea kuapata