Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akitembelea banda la Wizara ya Viwanda na Biashara kuona huduma zinazotolewa katika banda hilo.
Mhe. Simbachawene amefanya ziara hiyo Juni 17, 2025 na kupokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu, Bw. Said Mussa kabla ya kufungua wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.