Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mhe.Kasim Majaliwa ametoa rai wakulima nchini kutumia vyama vya ushirika ili kupata Masoko ya uhakika na yenye bei nzuri.


.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa ametoa rai wakulima nchini kutumia vyama vya ushirika ili kupata Masoko ya uhakika na yenye bei nzuri.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Maonesho ya Nanenane Agosti 03,2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Mhe.Majaliwa amesema Katika kipindi Cha miaka miwili ya 2023/ 2024 na 2025 nchi imeshuhudia mafanikio makubwa yanayodhihirisha nguvu ya ushirika katika kuleta tija kwenye sekta ya kilimo na kuinua maisha ya wananchi.

Aidha, ameeleza kuwa kwa kipindi hicho pembejeo za kilimo zenye thamani ya shilingi tirioni moja zimesambazwa kwa wakulima kupitia mfumo wa ushirika katika mikoa mbalimbali ambapo tani 3:8 zimesambazwa na kupatikana kiasi cha shilingi tirioni 6.2.

Kwa upande wake Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Dkt.Benson Ndiage ameusifu mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umekuwa ukitumiwa na vyama vya ushirika katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kuwa, hadi sasa vyama vya ushirika vimeuza mazoa yenye thamani shilingi tirioni 4 , huku akisema kuwa idadi ya mazao pia imeongezela na kufikia 14 kutoka matano ya awali.

Maonesho ya nanenane Kitaifa yanaendelea katika Viwanja vya Nzuguni jiji Dodoma ambapo kilele chake kitafanyika tarehe 8 Agosti 2025 ikiwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.