Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Hongereni CAMARTEC Kwa kuzalisha na kubuni Machine zinazowasaidia wakulima na wafugaji

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika amekipongeza Kituo cha zana za kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kwa kuzalisha na kubuni mashine, zinazowasaidia wakulima na wafugaji kuboresha shughuli zao na kupata masoko ya uhakika.

Amebainisha hayo wakati wa ziara ya kamati hiyo katika kituo hicho ambapo Mhe.Mwanyika amesema kazi inayofanywa na kituo hicho ni kubwa na ya kupongeza kwani wamejikita katika utafiti na kutengeneza zana mbalimbali za kilimo na mifugo ambazo zinatoa suluhisho kwa wakulima wa kawaida na wafugaji kwa kusaidia wakulima wengi ambao wapo zaidi ya asilimia 86 nchini.

Aidha amesema utafiti na utengenezaji wa zana hizo ni ukombozi kwa wakulima kwani katika kituo hicho wameona mashine za kila aina, zikiwemo trekta zenye uwezo wa kulima,kupanda,kuweka mbolea na zingine za kuvuna michikichi , kusaga nafaka na vyakula vya mifugo.

Vilevile Mhe.Mwanyika amesema kuwa Mashine hizo zilizotengezwa na Kituo hicho zinasaidia kuachana na uagizaji wa mashine za nje ya nchi, kutokana na utengenezaji wa mashine zinazoendana na jiografia ya nchi na kumuwezesha mkulima kununua mashine inayolingana na mazingira yake hivyo kama kamati watahakikisha wanafahamu changamoto zao, ili wakaishauri serikali kuzitatua changamoto hizo za kuwasaidia wakulima kwa kuwatengenezea mashine zinazoendana na mahitaji yao.

Naye Waziri wa Viiwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kwa dhamira njema ya Serikali inakiwezesha Kituo cha CAMARTEC ili kuhakikisha kilimo kinakua cha ufanisi na kuondoa changamoto ya kupoteza chakula baada ya kuvuna kwa kutumia mashine hizo.

"Hapa kuna mashine za kuchakata mabua na kuhifadhi kwa muda mrefu, hii inamsaidia mfugaji kutumia chakula hiki wakati wa uhaba wa chakula na hakuna chakula kinachopotea na hii inawezesha mifugo yetu kuwa bora yenye tija kwa sababu ya chakula chenye uhakika wakati wote,"amesema.

Dk.Kijaji ameongeza kuwa wanufaika wakubwa wa utengenezaji mashine hizo ni vijana wote waliomaliza vyuo vya kati na vyuo mbalimbali kupata ajira kwani mkulima anaponunzana za kilimo kwenda kijijni anamwitaji kijana huyu kuendesha mitambo hiyo