Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

JICA yapongezwa kwa ushirikiano na uhamasishaji ukuaji wa Viwanda nchini*


JICA yapongezwa kwa ushirikiano na uhamasishaji ukuaji wa Viwanda nchini*

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Needpeace Wambuya amelipongeza Shirika la Maendeleo la Watu wa Japani (JICA) kwa ushirikiano mkubwa unaoutowa katika kutoa ushauri wa kitaalam na uhamashijaji ukuaji wa Viwanda nchini.

Bw. Wambuya ameyasema hayo Februari 20, 2025 akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah katika ufunguzi wa Mkutano wa kuhitimisha Mradi wa Washauri wa Kitaalam wa JICA katika uwekezaji na maendeleo ya viwanda uliofanyika jijini Dodoma.

"Napenda kuchukua nafasi hii niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara kuishukuru (JICA) kwa mchango wao mkubwa wa kuhamasisha ukuaji Viwanda nchini pamoja na ushauri wa kitaalam ambao umekuwa ukitolewa kwa miaka mingi hapa Wizarani na katika nchi yetu" Amesema Wambuya.

Aidha Bw. Wambuya ametoa wito kwa Washiriki wa Mkutano huo kutoa michango yenye tija itakayoleta maendeleo katika sekta za uwekezaji , Viwanda na Biashara nchini wakati wa majadiliano.

Akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda Bi Aveline Mbunda
amesema kuwa Mkutano huo umeshirikisha Wadau kutoka sekta ya Viwanda na Biashara zikiwemo Wizara, Taasisi za umma, Mashirika, Wabia wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Maafisa Biashara kutoka Mikoa yote 25 ya Tanzania Bara ili waweze kijadili tafiti zao na kutoa matokeo chanya yanayolenga kukuza maendeleo ya Viwanda nchini.