Habari
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara,Kilimo, Mifugo na Uvuvi imeielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuwa na mpango mkakati endelevu wa utoaji Elimu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara,Kilimo, Mifugo na Uvuvi imeielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuwa na mpango mkakati endelevu wa utoaji Elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipimo.
Maelekezo hayo yanetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda ,Biashara ,Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika ( Mb) Novemba 21, 2023 wakati wa Semina ya kujenga uelewa kuhusu kazi na majukumu ya Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kwa Kamati hiyo na Mkoani Kagera
Aidha, Mwanyika ameelekeza Wizara kuwa na mkakati endelevu wa ukaguzi wa vipimo vinavyotumika katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuanza mara moja na upimaji katika maeneo ya muda wa maongezi na tax za mitandao, kwa kuwa maeneo hayo yanatumiwa sana na wananchi.
"Sisi kama Kamati ya Bunge tunaosimamia na kuishauri Serikali tunaielekeza Wizara muwe na zoezi endelevu la ukaguzi wa vipimo sahihi sambamba na utoaji elimu kuhusu uelewa hasa kwa wananchi wa chini ambao ndio walaji wa mwisho Ili kiasi cha fedha wanacholipa kiendane na kiasi cha bidhaa wanazonunua " Amesema Mwanyika.