Habari
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Mifugo na Kilimo imepokea taarifa ya Wizara

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Mifugo na Kilimo imepokea na kujadili Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya Mpango wa Serikali kwa Kipindi cha Julai-Desemba 2023/2024.
Kamati hiyo chini ya Kaimu Mwenyekiti Prof Patrick Ndakidemi imeipongeza Wizara hiyo kwa uwasilishaji wa taarifa yake iliyojitosheleza na kuishauri Wizara kuendelea kusimamia Taasisi zake na Sekta ya Viwanda na Biashara ili kuendelea kuleta tija kwa Taifa.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amesema lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan nikuhakikisha vipaumbele vya maendelo vinafikiwa kwa asilimia mia moja na na kama Wizara itaendelea kusikiliza na Kutekeleza maelekezo na ushauri wa kamati hiyo.
Aidha Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri Mhe Exaud Kigahe(Mb) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hashil T. Abdallah na Wakuu wa taasisi,Idara na Vitengo mbalimbali vya Wizara.
Kikao hicho kimefanyika Katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma, Januari 18,2024.