Habari
Kamati ya kudumu ya Viwanda, Biashara , Mifugo na Kilimo yapokea Taarifa ya FCC

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Mifugo na Kilimo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe Deudatus Mnyika imepokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu Utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Ushindani(FCC) ikiongozwa na Waziri wa Viwanda Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (Mb),Naibu Waziri Mhe Exhaud Kigahe (Mb) , Katibu Mkuu Dkt .Hashil Abdallah,
Aidha Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu Tume ya Ushindani Bw. Wiliam Erio na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara na Taasisi.
Kikao cha kuwasilisha Taarifa hiyo kimefanyika Januari 19,2024, Bungeni Dodoma.