Habari
Kampuni 18 za Kitanzania zimeanza kufanya biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA)
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Kampuni 18 za Kitanzania zimeanza kufanya biashara na zimepeleka biashara mara 17 kwenye nchi tano zilizopo katika ndani ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA)
Ameyasema hayo Desemba 6, 2023 katika ufunguzi wa Kongamano la Pili la Wanawake la Biashara la AfCFTA linalofanyika kuanzia tarehe 6-8 JNICC, Jijini Dar es salaaam
Aidha Amebainisha kuwa kati ya Kampuni hizo 18 tatu (3) ni Kampuni za wanawake ambazo ni pamoja na Ajat ltd, Mama Mia’s Soko na NatureRipe zote za Tanzania
“Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi na kushughulikia kero zote ili tuendelee kuwainua Wanawake” Amesema Dkt Kijaji.
“Tunawashukuru waandaaji wa Kongamano la AFCFTA ambalo linafanyika wakati Bara la Afrika linachukua hatua kubwa za kutekeleza Mkataba wa eneo huru la Biashara Afrika Mkataba huu ni fursa kubwa kwa wanawake na vijana katika sekta ya Biashara” -Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Ashatu Kijaji