Habari
Katibu Mkuu wa AfCFTA Mhe. Wamkele Mene mafanikio yamepatikana katika Maendeleo ya Itifaki ya Wanawake, Vijana na Biashara

Katibu Mkuu wa AfCFTA Mhe. Wamkele Mene amesema mafanikio yamepatikana katika Maendeleo ya Itifaki ya Wanawake, Vijana na Biashara ambapo Mawaziri wa Biashara watajadiliana kufikia makubaliano ambayo yatawasilishwa Februari 2024 katika Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali ili ithibitishwe.
Ameyasema hayo Desemba 6, 2023 katika ufunguzi wa Kongamano la Pili la Wanawake la Biashara la AfCFTA linalofanyika kuanzia tarehe 6-8 JNICC, Jijini Dar es salaaam
Aidha amebainisha kuwa Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya biashara zote barani Afrika ni biashara ndogo na za kati (SMEs), na asilimia 60 zinamilikiwa na wanawake, ambapo zinachangia asilimia 80 ya uzalishaji wa ajira na kuchangia asilimia 40 ya Pato la Taifa la Afrika kwa pamoja.
Vilevile amesisitiza kuwa ni muhimu kujua kwamba Itifaki ya Wanawake na Vijana katika nafasi za biashara inaweka Bara la Afrika kwa Wanawake katika biashara kunufaika kupitia maendeleo ya kiuchumi.