Habari
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, atembelea kiwanda cha chumvi cha Uvinza.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, atembelea kiwanda cha chumvi cha Uvinza. Leo tarehe 29 Septemba, 2020, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe ametembelea kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Uvinza kilichopo Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazoikabili kiwanda hicho na kuzifanyia kazi. katika ziara hiyo Katibu Mkuu aliambatana na maafisa wa Serikali kutoka Kigoma na maafisa kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) ambao walieleza namna bora ya upatikanaji wa soko la uhakika ndani na nje ya nchi.