Habari
Maandalizi ya Mkutano wa SCTIFI 43 ngazi ya Makatibu wa Wakuu wa EAC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundu akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha maandalizi kabla ya kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) ngazi ya Makatibu Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi , Congo DRC na Sudani Kusini kilichofanyika jijini Arusha tarehe 08 Februari 2024.
Ujumbe wa Tanzania ulijumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TANTRADE), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Tume ya Ushindani (FCC) na Mamlaka ya Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi.