Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Majadiliano kuhusu mchakato wa Itifaki ya Viwanda na eneo huru la Utatu


Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Manyama Bwire amekutana na kuzungumza na Dkt.Johnsein Rutaihwa, Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Viwanda Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Ujumbe alioambatana nao.

Bw. Manyama Bwire akiwa amemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, wamejadiliana kuhusu mchakato wa Iifaki ya Viwanda na Eneo Huru la Utatu.

Kikao kimefanyika Februari 01, 2024 katika ukumbi wa Wizara, Mtumba Dodoma.